Ngao ya taifa, Nafasi za kazi

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi mia nne sabini  (470) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili

 

1.0      AFISA MIFUGO DARAJA LA II (LIVESTOCK OFFICER II) – NAFASI 65

1.1      MAJUKUMU YA KAZI

  1. Kubuni mipango ya uzalishaji mifugo wilayani.
  2. Kuratibu uzalishaji wa mifugo katika mashamba madogo na makubwa ya mifugo. iii. Kusaidia kuratibu mipango ya ugani kuhusiana na uzalishaji wa mifugo wilayani.
  3. Kuratibu na kuendesha mafunzo ya ufugaji bora, usindikaji wa mazao ya mifugo kwa wataalam wa mifugo na wafugaji
  4. Kufanya mapitio na marekebisho ya miundombinu ya masoko ya mifugo wilayani na
  5. Kubuni, kuanzisha na kutekeleza miradi ya maendeleo ya mifugo wilayani.
  • Kufanya soroveya ya rasilimali (resource survey) k.m. mifugo, vyakula vya mifugo, malisho n.k. katika eneo lake la kazi.
  • Kuendesha mafunzo kwa mawakala, wauzaji na wataalam juu ya njia salama katika kuweka na kusambaza pembejeo za mifugo.
  1. Kutafiti maeneo mapya yanayofaa kwa ufugaji wa mifugo mbalimbali.
  2. Kufanya tathmini juu ya uharibifu wa mazingira unaotokana na ufugaji katika wilaya. xi. Kushiriki katika shughuli za kudhibiti milipuko ya wanyama/viumbe waharibifu wa malisho.
  • Kufuatilia, kuweka, kuchambua na kutafsiri takwimu za uzalishaji wa mifugo.
  • Kuandaa taarifa ya jumla juu ya maendeleo ya mifugo na xiv. Kufanya kazi nyingine zinazohusiana na fani yake kama atakavyoelekezwa na mkuu wake wa kazi.

1.2 SIFA ZA MWOMBAJI

 

Kuajiriwa wenye Shahada ya Sayansi ya Wanyama (Animal Science) au Sayansi ya Kilimo waliobobea katika Sayansi ya Wanyama kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine au kutoka chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

1.3 NGAZI YA MSHAHARA

Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali TGS D.

 

2.0 AFISA MIFUGO MSAIDIZI DARAJA LA II (LIVESTOCK FIELD OFFICER II)   NAFASI ZA KAZI  210

2.1   MAJUKUMU YA KAZI

  1. Kufanya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo kwa wafugaji wa eneo lake.
  2. Kwa kushirikiana na wakaguzi wa afya, atakagua nyama na usafi wa machinjio mara kwa mara. iii. Kukusanya takwimu za nyama na mazao yatokanayo na mifugo kama ngozi na kuandika ripoti.
  3. Kuratibu magonjwa ya mifugo chini ya usimamizi wa Daktari wa mifugo na kushauri wafugaji jinsi ya kukinga mifugo dhidi ya magonjwa.
  4. Kutembelea wafugaji mara kwa mara na kuwapa ushauri fasaha wa kitaalam katika eneo lake la kazi.
  5. Kukusanya takwimu zote za maendeleo ya mifugo katika eneo lake.
  • Kushauri na kusimamia ujenzi wa majosho, machinjio, vibanio na miundo mbinu inayohusiana na ufugaji bora.
  • Kusimamia uchanganyaji wa dawa ya josho. ix. Kuhusika na uhamilishaji na uzalishaji wa mifugo kwa ujumla.
  1. Kushauri wafugaji kuhusu mbinu bora za kuzalisha maziwa na utunzaji wa ndama na
  2. Kufanya kazi nyingine za fani yake kama atakavyopangiwa na mkuu wake wa kazi wa kazi.

 

2.2  SIFA ZA MWOMBAJI

 

Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV au VI wenye Stashahada (Diploma NTA Level 6) katika mojawapo ya fani zifuatazo:- Uzalishaji Mifugo; Uzalishaji Maziwa na Kuku; Afya ya Mifugo na Uzalishaji au Ukaguzi wa Nyama kutoka Vyuo vya Wakala wa Mafunzo ya Mifugo au kutoka chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

 

2.3 NGAZI YA MSHAHARA –

Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali TGS C.

 

3.0  FUNDI SANIFU WA MAABARA ZA UVUVI DARAJA II (FISHERIES  LABORATORY  TECHNICIAN II)  –  NAFASI 6

3.1 MAJUKUMU YA KAZI

 

  1. Kufanya uchunguzi wa sampuli za samaki na mazao ya uvuvi, maji, tope, na mazingira; ii. Kuandaa vifaa na vitendanishi (reagents) kwa ajili ya uchunguzi wa sampuli; iii. Kuhifadhi sampuli zinazotakiwa kufanyiwa uchunguzi au kupelekwa Maabara ya ; iv. Kuweka kumbukumbu za kimaabara. Kutunza vifaa vya maabara; v. Kufanya usafi wa maabara na vifaa vilivyotumika; vi. Kuteketeza mabaki ya sampuli na vitendanishi vilivyotumika kulingana na miongozo ya uteketezaji mabaki; na vii. Kufanya kazi nyingine za fani yake kama atakavyopangiwa na mkuu wake wa kazi.

3.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au VI wenye Stashahada (Diploma NTA – level 6) katika mojawapo ya fani za Chemistry, Food Science and Technology,Fisheries Management and Technology, Fish Processing, Laboratory Technology,Aquaculture, Aquatic Science kutoka Vyuo vya Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (Fisheries Education and Training Agency – FETA) au kutoka vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

3.3 NGAZI YA MSHAHARA : TGS. C

 

4.0 AFISA HABARI DARAJA LA II (INFORMATION OFFICER GRADE II) NAFASI 33

4.1 MAJUKUMU YA KAZI

  1. Kukusanya na kuandika habari; ii. Kupiga picha; iii. Kuamdaa picha za maonyesho; iv. Kuhifadhi picha na kuhudumia maktaba na marejeo; v. Kuandaa majarida na mabango(posters); vi. Kukusanya takwimu mbalimbali; na

vii. Kuandaa majarida na vipeperushi.

 

4.2  SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza au Stashahada ya juu ya Uandishi wa Habari kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.

4.3 NGAZI YA MSHAHARA:

Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D.

MASHARTI YA JUMLA.

 

  1. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini;
  2. Waombaji wenye uelemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma;
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa; Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  1. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika. vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
    • Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
    • Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
    • Computer Certificate
    • Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
  • “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  1. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  2. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  3. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
  • Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 10 Septemba, 2023.

 

MUHIMU:

Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;

KATIBU,

OFISI YA RAIS,

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

 

S.L.P. 2320 DODOMA.

  1. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;

http://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa Recruitment Portal’)

 

  1. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Tafadhali bofya hapa Public Service Recruitment Service (PSRS)  Kufanya maonbi sasa.

Tafadhali bofya hapa kuona nafasi za kazi nyingine zaidi zilizotangazwa Next