Ngao ya taifa, Nafasi za kazi

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi mia nne sabini  (470) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili.

9.0 MWANDAZI DARAJA LA II (WAITER) – NAFASI ZA KAZI 4

9.1 MAJUKUMU YA KAZI

  1. Kuandaa meza ya kulia chakula;
  2. Kupamba meza ya kulia chakula; iii. Kupanga vifaa vya kulia chakula mezani; na iv. Kuondoa vyombo baada ya kula chakula.

 

9.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Wenye cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV na kufuzu mafunzo si chini ya mwaka mmoja katika fani ya ‘Food and Bevarages’ yanayotolewa na chuo chochote kinachotambuliwa na serikali.

9.3 MSHAHARA:

Kwa kuzingatia ngazi ya mshahara ya Serikali yaani TGS B

 

10.0 MTUNZA NYUMBA DARAJA LA II (HOUSEKEEPER) NAFASI 3

10.1    MAJUKUMU YA KAZI

  1. Kuandaa vitanda; ii. Kuhakikisha usafi wa nguo (lines), mapazia na mazulia; na iii. Kusimamia utunzaji wa bustani na ukataji majani.

             

10.2    SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV au VI wenye Stashahada ya Home Economics au sifa inayolingana na hiyo kutoka kwenye Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali. wenye

 

10.3  MSHAHARA:

Kwa kuzingatia ngazi ya mshahara ya Serikali yaani TGS C.

 

11.0 MHUDUMU WA JIKONI DARAJA LA II (KITCHEN ATTENDANT) – NAFASI 4

11.1    MAJUKUMU YA KAZI

  1. Kusafisha vyombo vya kupikia; ii. Kusafisha vyombo vya kulia chakula; iii. Kusafisha meza itumiwayo kwa kulia chakula; iv. Kuwatayarishia wapishi/Waandazi vifaa vya Mpishi na Mezani; v. Kusafisha maeneo ya kulia chakula na kupikia; na vi. Kuwasaidia Waandazi na Wapishi.

 

11.2    SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa Wahitimu wa kidato cha Nne wenye cheti cha mafunzo ya Uhudumu wa Jikoni kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali..

 

11.3 MSHAHARA:

Kwa kuzingatia ngazi ya mshahara ya Serikali yaani TGS A  

 

12.0  MHIFADHI  WANYAMAPORI DARAJA  LA III (GAME WARDEN III) – NAFASI  4

12.1    MAJUKUMU YA KAZI

  1. Kufanya doria ndani na nje ya eneo la hifadhi.
  • Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi.
  • Kusimamia shughuli za uwindaji wa kitalii na utalii wa picha. iv. Kulinda binadamu na mali zake dhidi ya Wanyamapori. v. Kukusanya na kulinda Nyara za Serikali.
  1. Kufanya usafi na ulinzi wa kambi. vii. Kusimamia uingiaji na utokaji wa watu na mali zao kwenye hifadhi.
  • Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa ushahidi Mahakamani.
  1. Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya wanyamapori na kukusanya takwimu zao.
  2. Kusimamia taratibu za kusafirisha wanyamapori hai na Nyara ndani na nje ya nchi.
  3. Kudhibiti wanyamapori waharibifu. xii. Kudhibiti moto kwenye hifadhi na xiii. Kufanya kazi nyingine utakazopangiwa zinazoendana na taalima yake.

 

 

 

 

12.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au cha VI wenye Astashahada ya awali ya Uhifadhi wa Wanyamapori

(Basic Technician Certificate in Wildlife Management) kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na

Serikali au; Wahitimu wa Kidato cha Nne au kidato cha Sita wenye Astashahada ya Uhifadhi

Wanyamapori (Technician Certificate in Wildlife Management) kutoka Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

 

12.3 MSHAHARA:

Kwa kuzingatia ngazi ya mshahara ya Serikali yaani TGS B  

MASHARTI YA JUMLA.

 

  1. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini;
  2. Waombaji wenye uelemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma;
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa; Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  1. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika. vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
    • Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
    • Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
    • Computer Certificate
    • Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
  • “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  1. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  2. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  3. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
  • Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 10 Septemba, 2023.

 

MUHIMU:

Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;

KATIBU,

OFISI YA RAIS,

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

 

S.L.P. 2320 DODOMA.

  1. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;

http://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa Recruitment Portal’)

 

  1. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Tafadhali bofya hapa Public Service Recruitment Service (PSRS)  Kufanya maonbi sasa.

Tafadhali bofya hapa kuona nafasi za kazi nyingine zaidi zilizotangazwa Previous

Tafadhali bofya hapa kuona nafasi za kazi nyingine zaidi zilizotangazwa Next