Ngao ya taifa, Nafasi za kazi

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi mia nne sabini (470) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili.

13.0 MHIFADHI  WANYAMAPORI DARAJA  LA II (GAME WARDEN II) – NAFASI  5

13.1 MAJUKUMU YA KAZI

  1. Kufanya doria ndani na nje ya eneo la hifadhi.
  2. Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi.
  • Kusimamia shughuli za uwindaji wa kitalii na utalii wa picha. iv. Kulinda binadamu na mali zake dhidi ya Wanyamapori. v. Kukusanya na kulinda Nyara za Serikali.
  1. Kufanya usafi na ulinzi wa kambi. vii. Kusimamia uingiaji na utokaji wa watu na mali zao kwenye hifadhi. viii. Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa ushahidi Mahakamani.
  2. Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya wanyamapori na kukusanya takwimu zao.
  3. Kusimamia taratibu za kusafirisha wanyamapori hai na Nyara ndani na nje ya nchi.
  4. Kudhibiti wanyamapori waharibifu. xii. Kudhibiti moto kwenye hifadhi na xiii. Kufanya kazi nyingine utakazopangiwa zinazoendana na taalima yake

 

13.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au cha VI wenye Stashahada  ya Uhifadhi wa Wanyamapori (Diploma in Wildlife Management) kutoka chuo cha Wanyamapori na chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

13.3 MSHAHARA:

Kwa kuzingatia ngazi ya mshahara ya Serikali yaani TGS C.  

 

14.0 MSAIDIZI WA HESABU  DARAJA LA II (ACCOUNTS ASSISTANT II) – NAFASI 36

14.1 MAJUKUMU YA KAZI

  1. Kuandika na kutunza “Regester” zinazohusu shughuli za uhasibu;
  2. Kutunza kumbukumbu za hesabu;
  • Kupeleka barua/nyaraka za uhasibu benki; na iv. Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

 

14.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye cheti  cha Astashahada ya Uhasibu kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali au cheti cha ATEC I kinachotolewa na NBAA au sifa nyingine zinazolingana na hizo zinazotambulika na NBAA.

14.3 MSHAHARA:

Kwa kuzingatia ngazi ya mshahara ya Serikali yaani TGS B.  

 

 

15.0 AFISA MAENDELEO YA VIJANA DARAJA LA II (YOUTH DEVELOPMENT OFFICER II) – NAFASI 1

15.1  MAJUKUMU YA KAZI

  1. Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa sera ya vijana.
  2. Kuratibu shughuli za mikopo/mifuko ya vijana. iii. Kuhamasisha vijana ili kufufua moyo wa kujitolea nchini.
  3. Kupanga na kuendesha mafunzo yanayohusu stadi za maisha,stadi za kazi na afya ya vijana.
  4. Kukusanya takwimu mbalimbali zinazohusu vijana.
  5. Kuratibu shughuli mbalimbali za NGOs zinazoshughulikia masuala ya vijana.
  • Kuanzisha vituo vya ushauri nasaha, ajira kwa vijana na elimu ya familia kwa kushirikiana na vyama visivyo vya Serikali (NGO).
  • Kuandaa na kuboresha malezi ya vijana.
  1. Kuwahamasisha Waajiri na Wafadhili mbalimbali wachangie mfuko wa mikopo nafuu kwa Vijana katika maeneo mbalimbali.
  2. Kukuza na kuendeleza vipaji mbalimbali walivyonavyo vijana ili kuwawezesha kujiajiri na
  3. Kuandaa mipango wa kuwahamasisha vijana ili kuanzisha miradi midogomidogo ya kuajiri.

 

15.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu ya Maendeleo ya Vijana kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

16.0 AFISA KILIMO MSAIDIZI DARAJA LA III – NAFASI 30

16.1    MAJUKUMU YA KAZI

  1. Kushirikiana na wakulima kuendesha mashamba ya majaribio na mashamba darasa;
  2. Kutembelea wakulima/vikundi vya wakulima katika mashamba yao na kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya mbinu bora na za kisasa za kilimo cha kibiashara;
  • Kufundisha na kuelekeza wakulima juu ya matumizi bora ya mbolea, madawa na zana za kilimo;
  1. Kukusanya na kutunza takwimu za hali ya kilimo katika Kijiji;
  2. Kubuni na kuandaa vihenge vya kisasa vya hifadhi ya mazao na kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mazao;
  3. Kutoa taarifa juu ya dalili za kuwepo visumbufu vya mimea na mazao; vii. Kuandaa na kutumia daftari la kilimo katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku; viii. Kushiriki katika mchakato wa kuibua fursa na vikwazo vya maendeleo (Opportunities and Obstacles for Development (O & OD) na kuandaa mpango wa maendeleo ya kilimo wa kijiji (Village Agricultural Development Plan (VADP); na ix. Kuandaa taarifa ya utekelezaji ya kila mwezi kuiwasilisha kwa Afisa Ugani wa Kata na nakala kuiwasilisha kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji.

 

16.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa waliohitimu kidato cha nne wenye Astashahada ya Kilimo kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

16.3 NGAZI YA MSHAHARA:

Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B

MASHARTI YA JUMLA.

 

  1. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini;
  2. Waombaji wenye uelemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma;
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa; Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  1. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika. vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
    • Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
    • Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
    • Computer Certificate
    • Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
  • “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  1. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  2. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  3. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
  • Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 10 Septemba, 2023.

 

MUHIMU:

Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;

KATIBU,

OFISI YA RAIS,

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

 

S.L.P. 2320 DODOMA.

  1. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;

http://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa Recruitment Portal’)

 

  1. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Tafadhali bofya hapa Public Service Recruitment Service (PSRS)  Kufanya maonbi sasa.

Tafadhali bofya hapa kuona nafasi za kazi nyingine zaidi zilizotangazwa Previous

Tafadhali bofya hapa kuona nafasi za kazi nyingine zaidi zilizotangazwa Next