TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Halmashauri ya Wilaya ya Pangani imepokea kibali cha Ajira mpya kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma chenye Kumb. Na. cha Tarehe 11 Septemba, 2023.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani anawatangazia wananchi wote wenye şifa za kuomba nafasi ya kazi ya Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja II kama inavyooneka kwenye Tangazo hili.
MWANDISHI MWENDESHA OFİSİ II TGS. C (NAFASI 1)
SIFA ZA MWOMBAJI:
Awe na Elimu ya Kidato cha nne (Form IV) au Kidato cha sita (Form VI) aliyehitimu mafunzo ya stashahada/Diploma ya Uhazili au cheti cha (NTA level 6) ya uhazili, Aidha wawe wamefaulu somo la Hati mkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 (mia moja) kwa dakika moja na kupata program za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powerpoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambulika na serikali.
KAZI NA MAJUKUMU
- Kuchapa barua,taarifa na nyaraka za kawaida na şiri
- Kupokea wageni na kuwasaili shida zao , na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
- Kutunza taarifa za kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za mkuu wake na ratiba ya kazi zingine
- Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi
- Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika
Idara/kitengo/sehemu husika
- Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali; na Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.
S.L.P 89 Pangani, Simu 027 2977485, Barua Pepe: ded@panganidc.ao.tz, Tovuti: www.panganidc.go.tz
MASHARTI YA JUMLA YA WAOMBAJI WA NAFASI ZA KAZI
Waombaji wote wanatakiwa kuwa na sifa za jumla kama ifuatavyo:
- Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania
- Waombaji wote wawe na umri kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45
- Waombaji wote waandike barua zao za maombi wenyewe kwa mkono na aambatanishe Wasifu (CV), Vivuli vya Vyeti vyake vya Taaluma na Ujuzi, Cheti cha kuzaliwa na picha mbili za Passport size za hivi karibuni. Waombaji wote wawe na Namba ya kitambulisho cha Taifa (NIDA)
- Waombaji wenye vyeti vya kidato cha Nne cha Taaluma ambao vimepatikana nje ya Nchi wahakikishe vimehakikiwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) NA Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE).
- Waombaji waliofukuzwa Kazi, kupunguzwa au kuachishwa kazi katika Utumishi Wa Umma hawaruhusiwi.
- Waombaji ambao hawana sifa wanashauriwa kutokuomba kwa sababu barua zao hazitashughulikiwa
‘Testimonial” Provisional Statement” hati ya matokeo ya kidato cha Nne,Sita na Result Slip hazitapokelewa.
- Barua zote ziandikwe kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani kuanzia tarehe 15/09/2023 hadi 28/09/2023 saa 9.30 alasiri.
- Watakaochaguliwa kufanya Usaili watajulishwa Tarehe ya usaili.
Maombi yatumwe kwa anuani ifuatayo:-
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, S.L.P. 89,
PANGANI.
- Pia Tangazo hili linapatikana katika Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani panganidc.go,tz
- Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ajira.go.tz , Mbao za Matangazo.
MKURUGENZI MTENDÅJI
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
PANGANI
S.L.P 89 Pangani, Simu 027 2977485, Barua Pepe: ded@panganidc.go.tz, Tovuti: www.panganidc.go.tz