Breaking News

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi mia nne sabini (470) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili.

17.0 KATIBU WA KAMATI DARAJA LA II (COMMITEE CLERK)- NAFASI 10

17.1 MAJUKUMU YA KAZI

 1. Kuandaa ratiba ya vikao vyote vya Halmashauri na kushauriana na Mkurugenzi

Mtendaji; ii. Kuandaa Mihtasari ya vikao vya Halmashauri; iii. Kuweka kumbukumbu za vikao vya Halmashauri na Kamati zake; iv. Kutunza vifaa vyote vinavyohusiana na vikao;

 1. Kuhifadhi orodha ya mahudhurio ya Madiwani na Wataalam; vi. Kutoa ratiba ya ufuatiliaji na utekelezaji wa maazimio;

vii. Kutunza kanuni za mikutano; na viii. Kusimamia “cutting” za mikutano.

 

17.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Shahada /Stashahada ya Juu ya Sheria/Sanaa/ Utawala kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali

        17.3          NGAZI YA MSHAHARA:

Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D

 

18.0 DOBI DARAJA LA II – NAFASI 4

18.1 MAJUKUMU YA KAZI

 1. Kufanya uchambuzi wa nguo kwa ajili ya kuosha, kukausha, kunyoosha na kuzifungasha na ii. Kazi nyingine kama atakavyoelekezwa na Msimamizi wa kazi

 

18.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofuzu mafunzo ya miaka miwili au mitatu katika fani ya Dobi (Laundry Services) kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

 

18.3 NGAZI YA MSHAHARA:

Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B

 

19.0 DAKTARI WA MIFUGO DARAJA LA II (VETERNARY OFFICER II) – NAFASI 10

19.1 MAJUKUMU YA KAZI

 1. Kutoa huduma za afya ya mifugo.
 2. Kufanya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo katika eneo lake la kazi kwa mujibu wa sheria.
 • Kutayarisha na kusimamia mipango ya kuzuia, kudhibiti na kutokomeza magonjwa ya mifugo katika eneo lake.
 1. Kusimamia haki za wanyama.
 2. Kushiriki katika uchunguzi wa magonjwa ya wanyama pori katika eneo lake.
 3. Kusimamia na kuratibu uzingatiaji wa Kanuni na Sheria za Magonjwa, ukaguzi wa mifugo na mazao yake na pembejeo za mifugo.
 • Kuratibu na kusimamia shughuli za usafi wa machinjio na ukaguzi wa nyama katika eneo lake la kazi.
 • Kuandaa taarifa ya afya ya mifugo katika eneo lake la kazi na ix. Kufanya kazi nyingine zozote za fani yake atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

 

19.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Tiba ya Wanyama (Veterinary Medicine) kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) au kutoka Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali ambao wamesajiliwa na Baraza la Veterinari Tanzania.

 

19.3 NGAZI YA MSHAHARA:

Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS F

 

 

     20.0 AFISA MAENDELEO YA JAMII MSAIDIZI DARAJA LA II (ASSISTANT COMMUNITY DEVELOPMENT OFFICER) NAFASI – 2

20.1 MAJUKUMU YA KAZI

 1. Kuwezesha jamii kushiriki katika kubuni, kupanga, kutekeleza, kusimamia na kutathmini mipango/miradi ya maendeleo;
 2. Kutoa na kuwezesha upatikanaji wa mafunzo kwa viongozi wa Kijiji/mtaa na vikundi mbalimbali vya maendeleo kijijini/mtaa kuhusu utawala bora na uongozi, ujasiriamali. mbinu shirikishi jamii na kazi za kujitegemea;
 • Kuwa kiungo kati ya wananchi, viongozi na watumishi wengine wa Serikali katika kutekeleza shughuli za maendeleo;
 1. Kuwawezesha wananchi kupanga na kutekeleza kazi za kujitegemea katika ngazi ya Kijiji/mtaa;
 2. Kuandaa na kutoa taarifa za kazi za maendeleo ya jamii kila mwezi kwa uongozi wa kijiji na kwa

Msimamizi wake wa kazi;  vi.         Kusaidia kuunda vikundi vya kijamii na vya kimaendeleo;

 • Kutambua na kuwezesha kaya masikini kuinua uchumi wao kupitia fursa na rasilimali zinazowazunguka;
 • Kuwezesha utekelezaji wa afua za kuzuia ukatili wa jinsia;
 1. Kuwezesha utekelezaji wa program za uwezeshaji wanawake;
 2. Kuwezesha program za haki na malezi katika ngazi ya familia;
 3. Kuwezesha utekelezaji wa afua za kuzuia ukatili wa jinsia; na
 • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

   20.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au kidato cha sita, wenye Stashahada (Diploma) katika moja ya fani zifuatazo:- Maendeleo ya Jamii (Community Development), sayansi ya Jamii (Sociology), masomo ya Maendeleo (Development Studies), Mipango na Usimamizi wa Miradi (Project Planning and Management), Jinsia na Maendeleo (Gender and Development), Rural Development kutoka Vyuo vya Maendeleo ya Jamii au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

20.3 NGAZI YA MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C.

20.4 MLEZI WA WATOTO MSAIDIZI (CHILD CARE ASSISTANT) NAFASI -1

20.5 MAJUKUMU YA KAZI

 1. Kushiriki kutekeleza mpango jumui wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya watoto, (ECD integrated plan);ii. Kuandaa na kutekeleza ratiba ya shughuli za kila siku katika kituo husika;iii. Kubainisha na kutumia mazingira salama ya kujifunzia watoto;iv. Kutoa rufaa ya masuala ya watoto yaliyo nje ya uwezo wake;
 2. Kutambua watoto wenye mahitaji maalumu na kutoa huduma stahiki;vi. Kushiriki katika uhamasishaji wa jamii katika kutoa huduma za malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto;vii. Kutoa ushauri kwa wazazi/walezi kuhusu malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya watoto katika eneo lake;viii. Kuandaa na kutoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za kila siku katika eneo husika;ix. Kushiriki kwenye mchakato wa uendeshaji wa mashauri ya watoto katika ngazi husika (case management);
 3. Kuandaa taarifa ya uanzishaji wa vituo vya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto katika maeneo husika; naxi. Kufanya kazi nyingine yoyote atakayopangiwa na Mkuu wake wa kazi kulingana na elimu na ujuzi wake.

20.6 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au kidato cha sita waliohitimu mafunzo ya Astashahada katika mojawapo ya fani zifuatazo:-  Elimu ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto, Ustawi wa Jamii, Saikolojia au fani nyingine zinazofanana na hizo kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali.

20.7 NGAZI YA MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B.

 

MASHARTI YA JUMLA.

 

 1. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini;
 2. Waombaji wenye uelemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma;
 • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa; Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
 1. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika. vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
  • Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
  • Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
  • Computer Certificate
  • Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
 • “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
 • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
 1. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
 2. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
 3. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
 • Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 10 Septemba, 2023.

 

MUHIMU:

Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;

KATIBU,

OFISI YA RAIS,

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

 

S.L.P. 2320 DODOMA.

 1. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;

http://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa Recruitment Portal’)

 

 1. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Tafadhali bofya hapa Public Service Recruitment Service (PSRS)  Kufanya maonbi sasa.

Tafadhali bofya hapa kuona nafasi za kazi nyingine zaidi zilizotangazwa Previous

Check Also

nafasi za kazi pangani

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA PANGANI

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI Halmashauri ya Wilaya ya Pangani imepokea kibali cha Ajira mpya …