Ngao ya taifa, Nafasi za kazi

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi mia nne sabini  (470) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili

5.0 MSAIDIZI WA MISITU DARAJA LA II – NAFASI 21

5.1 MAJUKUMU YA KAZI

  1. Kukusanya mbegu; ii. Kuhudumia na kutunza bustani za miti;

iii. Kutunza na kuhudumia miti na misitu; na iv. Kufanya doria.

 

5.2  SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne au Sita wenye Astashahada (Cheti) ya Misitu kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

5.3 NGAZI YA MSHAHARA:

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani TGS B.

 

6.0       MSAIDIZI WA UVUVI – NAFASI 4

6.1      MAJUKUMU YA KAZI

  1. Kutoa huduma ya ugani kwa Wavuvi ikiwa ni pamoja na matumizi sahihi ya zana za uvuvi.
  2. Kukusanya takwimu na kutunza kumbukumbu za uvuvi na kutoa taarifa.
  • Kutoa ushauri kwa vikundi vya usimamizi wa rasilimali za uvuvi. iv. Kuhakiki usajili wa vyombo na matumizi ya zana za uvuvi na kutoa taarifa.
  1. Kukagua leseni za uvuvi kutokana na eneo alipo.
  2. Kuandaa na kusimamia mafunzo ya ugani katika uvuvi kwa vitendo. vii. Kufanya doria katika eneo lake.
  • Kushiriki katika shughuli za Utafiti na
  1. Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na fani yake.

6.2  SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV au VI ambao wamepata mafunzo ya Uvuvi na kutunukiwa Astashahada ya Uvuvi (NTA Level 5) kutoka Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (Fisheries  Education and Training Agency – FETA) au kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

6.3 NGAZI YA MSHAHARA:

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani TGS B

 

7.0 MPISHI II NAFASI 15

7.1  MAJUKUMU YA KAZI

  1. Kupika vyakula vya aina mbalimbali;
  2. Kutayarisha orodha ya vyakula vya mlo kamili (Balanced Diet); iii. Kuhakikisha vyombo vya kupikia vyakula vinakuwa safi; na iv. Kufanya kazi nyingine atakazoagizwa na Msimamizi wa kazi.

7.2  SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV waliofuzu mafunzo ya cheti yasiyopungua mwaka mmoja katika fani ya “Food Production” kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

7.3  MSHAHARA: TGS C

 

 

 

8.0        FUNDI SANIFU MIFUMO YA MAJI DARAJA LA II (PLUMBER) NAFASI 2

8.1      MAJUKUMU YA KAZI

  1. Kuhakiki uwezo wa kisima kutoa maji; ii. Kukagua na kufanya matengenezo ya mifumo ya maji katika majengo ya Ofisi; iii. Kukusanya na kukagua takwimu za maji; iv. Kuchora ‘hydrograph’ ya maji; na
  2. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na msimamizi wake wa kazi zinazoendana na sifa na fani yake.

8.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa vyuo vya Ufundi vinavyotambuliwa na Serikali ambao wana cheti cha ufundi (FTC) katika fani ya mifumo ya maji na wenye uwezo wa kutumia Kompyuta.

8.3 MSHAHARA: TGS. C

MASHARTI YA JUMLA.

 

  1. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini;
  2. Waombaji wenye uelemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma;
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa; Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  1. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika. vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
    • Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
    • Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
    • Computer Certificate
    • Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
  • “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  1. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  2. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  3. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
  • Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 10 Septemba, 2023.

 

MUHIMU:

Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;

KATIBU,

OFISI YA RAIS,

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

 

S.L.P. 2320 DODOMA.

  1. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;

http://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa Recruitment Portal’)

 

  1. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Tafadhali bonyeza hapa Public Service Recruitment Service (PSRS) ili kuomba kazi.

Bonyeza hapa kuangalia nafasi nyingi zaidi TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI 

Tafadhali bofya hapa kuona nafasi za kazi nyingine zaidi zilizotangazwa Next